24/7 Support: +255 756 556 556

info@faithvictorytz.org

24/7 Support: +255 756 556 556

info@faithvictorytz.org

KUMSIFU NA KUMTUKUZA MUNGU KILA SIKU

  • August 8, 2020

ZABURI 145 :1-3

 

Nitakutukuza wewe, Mungu wangu Mfalme, nitalisifu Jina lako milele na milele. Kila siku nitakusifu na kulitukuza Jina lako milele na milele. BWANA ni mkuu, anayestahili kusifiwa sana, ukuu wake haupimiki.

 

Wazo Kuhusu Neno la Leo

 

Namna tunavyomsifu Mungu milele, namna tunavyo heshimu ahadi zetu kumpa Mungu utukufu siku zote za maisha yetu, ni rahisi: ni kuyafanya hayo kila iitwapo leo. Ilimradi tunamtukuza Mungu leo, kumsifu milele inakuwa jambo la kawaida. Hivyo, unapoamua kulisifu na kulitukuza Jina la Mungu katika umilele kumbuka mahali unapopaswa kuanza kufanya hivyo: msifu na mtukuze Mungu leo ​​- si tu katika mambo unayosema, lakini pia kwa namna unavyoishi! Kumbuka, namna unavyoishi ni kielelezo na kitambulisho tosha kwa ulimwengu kutambua kama unamsifu na kumtukuza Mungu. Matendo yako yanazungumza zaidi kuliko maneno yako.

Maombi Yangu

Mungu mwenye nguvu na Baba mwenye upendo, leo nataka kukuambia namna ninavyoamini ulivyo wa ajabu. Wewe ni Mungu mwenye haki, mwaminifu, mtakatifu na mwenye huruma. Wewe ni Mungu wa upendo; na bado ni mwenye utukufu na nguvu zako hazilinganishwi na chochote duniani na hata mbinguni. Umenikomboa kutoka dhambini na kunipa matumaini dhidi ya kifo na mauti. Umeyajaza maisha yangu kwa kunipa watu wema walionizunguka na umeniahidi uzima wa milele pamoja nawe baada ya maisha haya ya duniani. Wewe, Ee Mungu, huna wa kulinganishwa naye na huna mpinzani. Wewe ni mfalme wangu, Mungu wangu, Baba yangu wa ajabu, mtukufu na mtakatifu. Katika jina la Yesu Kristo, nakuabudu na kukusifu leo na milele yote. Amina.

 

© Pastor Christine Mlingi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *