Mithali 9:10 (NENO)
“Kumcha BWANA ndicho chanzo cha hekima, na kumjua Aliye Mtakatifu ni ufahamu.”
Wazo Kuhusu Neno la Leo
Tunatafuta hekima katika maeneo mengi yasiyofaa. Lakini hekima ya kweli na ya kudumu inapatikana tu pale tunapoazimia kujinyenyekeza mbele ya Mungu wetu wa ajabu, kumpatia Yeye heshima na ibada anayostahiki.
Maombi Yangu
Mungu wangu wa ajabu na wa kushangaza, ukubwa wa uumbaji wako na uajabu wa vitu vitu ulivyoviumba, kazi ya mikono yako, vinanifanya ninyenyekee kimya katika kukuabudu Wewe. Tafadhali nisamehe upumbavu wangu unaonipeleka katika kiburi. Naomba uniongoza kwenye njia ya hekima yako. Katika Jina la Yesu Kristo ninaomba na kuamini. Amina.
© Pastor Christine Mlingi