24/7 Support: +255 756 556 556

info@faithvictorytz.org

24/7 Support: +255 756 556 556

info@faithvictorytz.org

KILA MTU NA AMHESABU MWENZIWE KUWA BORA

  • August 4, 2020

WAFILIPI 2 :3-4

 

“Msitende neno lolote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine.”

 

Wazo Kuhusu Neno la Leo

 

Unakumbuka moja ya maswali ya kwanza mwanadamu kuulizwa na Mungu kurekodiwa katika Biblia? “Yuko wapi Habili ndugu yako?” Ambapo Kaini alijibu: “Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?” (Mwanzo 4:9). Jibu la Paulo ni wazi na lisilopingika kwamba tuna wajibu wa kuujua na kuufuatilia mustakabali wa ndugu yako. Tuna wajibu wa kujishughulisha na mambo ya wengine zaidi ya kujishughulisha na mambo wetu wenyewe tu. Mwanadamu ni kiumbe anayeishi katika jamii na kwa sababu hiyo, tuna wajibu wa kutunzana na kuchukuliana katika maisha yetu ya kila siku, kama jamii moja.

Maombi Yangu

Baba, nifundishe namna bora ya kuipenda familia yako kama wewe unavyotupenda. Mara nyingi ninajishughulisha zaidi na mambo yangu mwenyewe hata nasahau wajibu wangu wa kuwahudumia wale walio na mahitaji, maumivu, mateso na changamoto mbalimbali wanaonizunguka. Nisaidie kukua zaidi na kufahamu zaidi mahitaji hayo ili uweze kuwahudumia kupitia mimi. Katika jina lenye nguvu la Yesu Kristo ninaomba na kuamini. Amina.

 

© Pastor Christine Mlingi

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *