24/7 Support: +255 756 556 556

info@faithvictorytz.org

24/7 Support: +255 756 556 556

info@faithvictorytz.org

FURAHINI KATIKA BWANA SIKU ZOTE

  • August 1, 2020

WAFILIPI 4 :4

“Furahini katika BWANA siku zote; tena nasema, Furahini.”

Wazo Kuhusu Neno la Leo

Furaha inapatikana katika Bwana Yesu Kristo, si katika vitu. Furaha inapatikana kwa kutambua kwamba Yesu yuko nawe kila dakika, anakupigania, anakusaidia, anakulinda, na anakutegemeza. Ninawezaje nisifurahi katika BWANA? Mungu ananipenda mno kiasi kwamba aliacha uungu wake na hazina yake kuu mbinguni ili nipate kushiriki naye katika utukufu wake kwa kuwa mwana wake. Furaha ni yangu kwa sababu ya neema yake.

Maombi Yangu

Baba yangu wa thamani, asante kwa kuwa daima uko pamoja nami na unajua kile kilicho moyoni mwangu na kunitunza kwa njia ambazo siwezi kufikiri hata kidogo. Ninatamani kukujua zaidi ili niweze kushiriki katika furaha isiyo na kifani ya mbinguni pamoja nawe. Hadi wakati huo, ninafurahi kweli kwa sababu ninajua kwamba hatima yangu iko salama mikononi mwako! Asante; katika Jina la Yesu Kristo Bwana wangu. Amina.

© Pastor Christine Mlingi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *