24/7 Support: +255 756 556 556

info@faithvictorytz.org

24/7 Support: +255 756 556 556

info@faithvictorytz.org

ENENDA KWA IMANI NA SI KWA KUONA

  • July 27, 2020

Hakuna kitu kinachouma sana kama kujikwaa kidole chako gizani. Uchungu unaoupata kwa dakika kadhaa ni mkubwa sana.  Mara nyingi tunajikwaa kwa sababu labda hatukuwa waangalifu sana wakati tunatembea. Kutembea na Yesu kila siku ni kuwa na imani naye na kujiaminisha kwamba tuko katika mustakabali sahihi, hata pale ambapo hatujui kwa uhalisia kitu kitakachotokea baada ya hapo. Hii ni kwa sababu, tunapaswa tutembee kwa imni na siyo kwa kuona.

 

USIPELEKWE NA UPEPO

 

Kama binadamu, mara nyingi tunafanya maamuzi yetu kwa kusukumwa na kile tunachoona. Kwa Mkristo, tunapaswa kuwa na mtazamo tofauti. Wakati wengine wakisukumwa kufanya jambo kwa kutegemea kile wanachoona, sisi tunapaswa kusukumwa na imani ndani ya Yesu Kristo. Uhusiano wetu na Yesu unapaswa kuzingatia imani yetu. Kilichoko mbele yetu kinaweza kuonekana ni kitu cha kutisha, lakini tunahitaji kuamini kwamba Yesu atatupigania na kutushindia na hivyo tunapaswa kusonga mbele.

 

Labla unakabiliwa na jambo ambalo unapaswa kufanya maamuzi. Kibinadamu na kwa mazingira ya kawaida unaona haiwezekani, lakini kama Roho Mtakatifu anakusukuma kwa ndani kwamba ulifanye jambo hilo, basi hupaswi kusita, msikilize Roho Mtakatifu, hata kwa mazingira yanayoonyesha kibinadamu haiwezekani.

 

Ndivyo ilivyokuwa katika simulizi katika Hesabu 13:1-33 na Hesabu 14:1-45. Kati ya wapelelezi 12 waliotumwa na Musa kwenda kupeleleza Kanaani, wawili tu yaani Kalebu na Yoshua ndio walioona na kuamini kwamba wanaweza kuwashinda waamaleki, lakini wengine wote 10 wakasema “…tulifika nchi ile uliyotutuma, na hakika yake, ni nchi yenye wingi wa maziwa na asali, na haya ndiyo matunda yake. Lakin watu wanaokaa katika nchi ile ni hodari, na miji yao ina maboma, nayo ni makubwa sana; na pamoja na hayo tuliwaona wana wa Anaki huko….. Hatuwezi kupanda tupigane na watu hawa; kwa maana wana nguvu kuliko sisi. … ile nchi tuliyoipita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi inayowala watu wanaoikaa; na watu wote tuliowaona ndani yake ni watu warefu mno. Kisha, huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi.” (Hesabu, 13:27-28; 31-33).

 

Tunatambua kwamba, hatimaye Israeli walikwenda wakapigana nao na wakawashinda maana Mungu alikuwa pamoja nao.

ENENDA KWA IMANI

 

Tunaendaje kwa imani? Inaanza kwa kuelewa nguvu na uweza wa Mungu. Yeye ana udhibiti na ana njia zote zinazohitajika kutulinda na kutupatia haja za mioyo yetu. Kisha, tunahitaji kuondoa hofu. Biblia inatuambia “Usiogope” Mara mia tatu na sitini na tano (365). Kwa maana nyingine, kila siku Mungu anakuambia, USIOGOPE. Na mara nyingi neno “Usiogope” katika Biblia linafuatiwa na Neno “Mimi nipo pamoja nawe.”

 

Hatimaye, tunahitaji kuamini kwamba mipango ya Mungu ni bora zaidi kuliko chochote tunachoweza kubuni. Ikiwa wewe ni mtu ambaye mara nyingi unakuwa mwangalifu sana katika kufanya mambo yako, na wakati wote unasubiri mazingira yote yawe sahihi kabla hujaamua kufanya jambo fulani, basi unahitaji kumwomba Mungu akuongezee imani.

 

Mungu akubariki.

 

 

© Pastor Christine Mlingi

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *