24/7 Support: +255 756 556 556

info@faithvictorytz.org

24/7 Support: +255 756 556 556

info@faithvictorytz.org

Kesho Yenye Ushindi .

By Pastor Christine Mlingi

Ni mara ngapi umejitamkia kuwa kesho yangu itakuwa bora na unatamani kuiona na kuiishi kwa sababu ni bora? Unaweza usielewe ninacho kizungumza kwa sababu leo yako imekua mbaya na hivyo unaona hata kesho yako itakua sio nzuri. Mithali 13:12 (NENO) inasema, “Kilichotarajiwa kikikawia kuja, moyo huugua, bali haja ya mtu ikipatikana, ni mti wa uzima.”

Ni kweli ndio maana unahitaji sana kuweka imani kama leo yangu imekuwa mbaya basi kesho yangu itakuwa nzuri kwa sababu kama kesho yako inafanana na leo yako hakuna maana ya Mungu kuitangaza kesho yako iwepo na wewe uwe mzima na hai.

Mungu anapokulinda na kukutunza anataka uone utukufu wake kwenye maisha yako hata kama mazingira yanakatisha tamaa. Kuna kila sababu ya Mungu kuifanya kesho yako kuwepo ndio maana imani ni jambo la msingi sana kwa mwanadamu. Na hivyo ndivyo inafaa mtu aamini ikiwa leo nilikuwa na huzuni basi kesho yangu iwe yenye furaha kwa sababu Mungu alituumba ili tuwe wenye furaha. Mithali 17:22 inasema, “Moyo uliochangamka ni dawa nzuri.”

Mara zote ukitaka kuiona kesho yako ni bora kuwa na mpango wa leo, na kesho yako, halafu mkabidhi Mungu leo, na kesho yako, na kumuomba Mungu ulinzi wa kuilinda kesho yako. Kwa kufanya hivyo unatengeneza muongozo wako na wa Mungu kushirikiana nawe badala ya kuamka siku inaanza kwa kufanya chochote kinachokuja mbele yako halafu hata Mungu anakushangaa. Unawezaje kupanga mambo yako bila Yeye kukusaidia?

Panga mambo ambayo unatakiwa kuyakamilisha au kuyafanya kesho pamoja na Mungu.

Biblia inasema katika kitabu cha Mithali 24:5 “…mtu wa maarifa huongeza uwezo.” Hivyo maarifa ndio nguvu inayokupatia uwezo wa kupanga mambo yako kabla hujayafanya. Kama Mungu alikupatia maarifa basi usiache kumwambia akusaidie katika mambo yako yote kwa sababu hujawahi weza jambo lolote hapa duniani bila msaada wake. Panga kesho yako yenye ushindi na uweze kufikia mafanikio yako na kwa msaada wa Bwana utatenda mambo makuu ukiamini.

&source=">