24/7 Support: +255 756 556 556

info@faithvictorytz.org

24/7 Support: +255 756 556 556

info@faithvictorytz.org

BWANA ATAKULINDA DHIDI YA MADHARA YOTE

  • July 29, 2020

Zaburi 121:7-8 (NENO)

“BWANA atakukinga na madhara yote, atayalinda maisha yako, BWANA atakulinda unapoingia na unapotoka, tangu sasa na hata milele.”

Wazo Kuhusu Neno la Leo

 

Zaburi ya 121 inahitimishwa na ahadi nzuri ya Mungu atunzaye maagano yake. Neno “kukinga” linamaanisha “kulinda, kutunza, au kushughulika nawe kwa uangalifu.” Kulinda huku kunahusisha ulinzi wa Mungu juu ya watu wake wakati walipokuwa wakienda Yerusalemu lakini kuna maana zaidi ya hiyo. Ni ulinzi unaohusisha maeneo manne:

 

Ulinzi dhidi ya mabaya (uovu).

Ulinzi wa maisha yetu.

Ulinzi tutokapo na tuingiapo.

Ulinzi wa milele yote.

 

Ni ahadi ya namna gani hii! … Katika Mungu, tuna anayetulinda dhidi ya kila aina ya uovu! Hakuna eneo la maisha yetu ambalo hahusiki nalo katika kutulinda. Jicho lake la ulinzi linatutazama wakati wote (Zaburi 33:18-19 NENO “Lakini macho ya BWANA yako kwa wale wamchao, kwa wale tumaini lao liko katika upendo wake usio na kikomo, ili awaokoe na mauti, na kuwahifadhi wakati wa njaa).” Haijalishi msimu, aidha tuingiapo au tutokapo, mchana au usiku, Yeye daima yupo kutulinda na kututunza. Ulinzi huu hauna tarehe ya kwisha muda wake, kwa sababu ulinzi wake ni wa milele yote. Tunainua macho yetu kuitazama milima na kukumbuka mahali msaada wetu unapotoka: unatoka kwa BWANA mlinzi wetu, (Zaburi 121:1-2) na ni tumaini hili na kweli hii inayotuhifadhi tangu sasa na hata milele.

Maombi Yangu

Ewe Mungu wangu, nakushukuru kwa sababu wewe ni mwema sana kwangu. Unanilinda na kunitunza daima. Haijalishi mazingira, changamoto, mateso na shida mbalimbali ninazopitia, umesema kupitia Neno lako kwamba uko pamoja nami siku zote. Umesema katika Isaya 49:16 (NENO) kwamba: “Tazama, nimekuchora kama muhuri katika vitanga vya mikono yangu, kuta zako zi mbele yangu daima.”   Aidha umesema kupitia Zekaria 2:8 (NENO) kwamba: “…kwa kuwa yeyote awagusaye ninyi, anaigusa mboni ya jicho lake, hakika nitauinua mkono wangu dhidi yao ili watumwa wao wawateke nyara …” Nakushukuru kwa sababu siku zote niko salama katika mikono yako. Naomba yote haya katika Jina la Yesu Kristo. Amina.

© Pastor Christine Mlingi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *