24/7 Support: +255 756 556 556

info@faithvictorytz.org

24/7 Support: +255 756 556 556

info@faithvictorytz.org

AMRI KUU: UPENDO

  • July 28, 2020

MATHAYO 22:37-39 (BHN)

“Yesu akamjibu ‘Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote na kwa akili yako yote.’ Hii ndiyo amri kuu na ya kwanza. Ya pili inafanana na hiyo: ‘Mpende jirani yako kama unvyojipenda wewe mwenyewe.’”

Wazo Kuhusu Neno la Leo

Jambo kuu tunalopaswa kulizingatia, baada tu ya Yesu Kristo, ni jinsi tunavyotendeana sisi kwa sisi. Matendo yetu yanasaliti mioyo yetu, kwa mema au mabaya, na ikiwa tunawatendea wengine na hata kuwaheshimu wengine kuliko sisi wenyewe, basi tunatimiza amri kuu ya kumpenda jirani yetu kama tunavyojipenda wenyewe (Yakobo 2: 8). Bila shaka hatuna tatizo la kujipenda wenyewe. Tunajitunza na kujipa vilivyo bora; lakini swali ni je, tunawatendea wengine kwa njia hiyo hiyo? Amri ya kwanza na kubwa ni kumpenda Mungu (Mathayo 22:37), “Na pili ni sawa na hivyo: ‘Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe'” (Mathayo 22:39). 1 Yohana 2:9-11 inatuambia kwamba hatuwezi kusema tunampenda Mungu wakati hatuwapendi ndugu zetu (au jirani zetu). Luka 6:1-11 ni mfano mzuri wa sio tu jinsi tunavyotendeana sisi kwa sisi lakini pia namna tunavyowatendea hata wale ambao ni adui zetu.

Maombi Yangu

Mungu Baba, kupitia Jina la Yesu Kristo, naomba uniumbie ndani yangu, roho ya upendo. Ule upendo wa agape usiohesabu mabaya. Upendo ule ambao uliufundisha kwamba tuwapende hata maadui zetu na tuwaombee. Upendo ule uliokufanya umtume mwana wako wa pekee, Yesu Kristo, kuja duniani kutufilia pale msalabani hata pale tulipokuwa tungali wenye dhambi, tumekuasi wewe. Ee, Mungu wangu, zaidi ya yote, unisaidie nikupende wewe na kuyatenda yaliyo mapenzi yako. Naomba yote haya kwa Jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo. Amina.

© Pastor Christine Mlingi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *